To Advertise here call +255786419829

To Advertise here call +255786419829

Wahitimu wasema, jeshi la akiba si kwa ajili ya CCM



Mkuu wa Wilaya ya Moshi Kipi Warioba.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi Kipi Warioba. 
Moshi. Vijana wametakiwa kuondokana na dhana kwamba Jeshi la Akiba lipo kwa ajili ya Chama cha Mapinduzi (CCM) jambo linalosababisha mwamko mdogo wa kujiunga na mafunzo ya jeshi hilo mkoani Kilimanjaro.
Wahitimu wa mafunzo ya jeshi hilo, kikosi namba 47 mwaka 2017 Manispaa ya Moshi walisema hayo katika risala iliyosomwa na askari wa kikosi hicho, Jackline Mmassi.
Akisoma risala hiyo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Moshi Kipi Warioba, Mmassi alisema dhana hiyo imekuwa chanzo cha vijana wengi kutokujiunga na mafunzo ya jeshi.
“Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa, ipo dhana iliyojengeka kuwa jeshi hili ni kwa ajili ya CCM jambo ambalo kwetu limekuwa changamoto kutokana na askari wa kikosi hiki kutohusika na chama chochote cha siasa,” alisema.
Askari hao waliiomba Serikali kutoa kipaumbele katika ajira sambamba na kujiunga na vikosi vya majeshi likiwamo Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Magereza na Uhamiaji.
“Tunauomba Mkoa kushawishi kampuni na taasisi mbalimbali kuwaajiri vijana waliohitimu mafunzo badala ya kuajiri ambao hawana ujuzi wowote wa silaha na kukabiliana na uhalifu,” alisema Mmassi.
Awali, Mkuu wa Wilaya ya Moshi Warioba alipiga marufuku kampuni na taasisi binafsi kuajiri vijana ambao hawajapitia mafunzo hayo.
“Ninawapa mwaka mmoja wote ambao wanafanya kazi kwenye kampuni binafsi na hawajapitia mafunzo ya jeshi la akiba, kujiunga na mafunzo hayo kabla sijaanzisha operesheni ya kuwasaka,” alisema.
Kuhusu shereha za miaka 56 Uhuru, alisema Sikukuu hiyo iliyofanyika jana ni kumbukizi ambayo kila Mtanzania anapaswa kuonyesha heshima na kufanya kazi kwa bidii.
“Pamoja na kufunga mafunzo ya askari wa akiba, maadui wakubwa wa Uhuru wetu ni uvivu, uzembe na kutokuwajibika. Kila mmoja kwa nafasi yake afanye kazi na kutofautisha siasa na kazi,” alisema Warioba.
Akizungumza na gazeti hili, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi alisema jeshi hilo halina uhusiano na chama hicho
Wahitimu wasema, jeshi la akiba si kwa ajili ya CCM Wahitimu wasema, jeshi la akiba si kwa ajili ya CCM Reviewed by EXUPER ASSOCIATION on December 09, 2017 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.