To Advertise here call +255786419829

To Advertise here call +255786419829

Wapalestina hawataki mazungumzo na Marekani

PalestineHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMike Pence hakaribishwi Palestine
Marekani imeionya Palestina dhidi ya maamuzi yake kutotaka kukutana na makamu wa rais Marekani ,Mike Pence katika kikao ambacho kilipangwa kufanyika mapema mwezi huu ili kujadili uamuzi wa rais Trump wa kuhamishia Yerusaleam kuwa mji mkuu wa Israel.
Ikulu ya Marekani imesema, uamuzi huo uliofikiwa na Palestina utakuwa hauna maana kwa kuwa hawataweza kupata suhulu ya mgogoro huo.
Makamu wa rais wa Marekani ana mpango wa kwenda katika ukanda huo wa mashariki ya kati lakini kiongozi wa ngazi za juu wa Palestina ,Jibril Rjoub amesema kuwa kiongozi huyo hakaribishwi Palestina.
Hatua hiyo imekuja mapema baada ya rais Trump kutangaza kuwa anautambua mji wa Yerusaleum kuwa mji mkuu wa israel,
Ambapo mpaka sasa Wapalestina takriban 31 wamejeruhiwa katika makabiliano yaliyozuka Ukanda wa Gaza na maeneo ya Ukingo wa Magharibi yanayotawaliwa na Israel kuhusu mji wa Jerusalem.
Wapalestina hawataki mazungumzo na Marekani Wapalestina hawataki mazungumzo na Marekani Reviewed by EXUPER ASSOCIATION on December 07, 2017 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.