To Advertise here call +255786419829

To Advertise here call +255786419829

Maiti za wanaume watatu zimekutwa pembezoni mwa Bahari ya Hindi eneo la Coco Beach ambapo kati ya hizo moja imekutwa na jiwe kubwa lililofungwa na kamba. Wafanyabiashara wa mihogo wa eneo hilo wamesema juzi wakiwa kwenye biashara zao asubuhi ghafla waliona maiti moja ikielea karibu na miti aina ya mikoko ikiwa na jiwe lililofungwa kifuani huku mikono yake ikifungwa na kamba. Mmoja wa wafanyabiashara, Aziza Ally amesema baada ya kuona maiti hiyo walitoa taarifa polisi ambapo walifika saa 4 asubuhi na kuichukua kwenye gari lao. Amesema ilipofika saa 8 mchana waliona maiti mbili kila moja ikiwa kwenye kiroba zikielea ndipo mmoja wao alitoa taarifa polisi baadaye zilichukuliwa. "Polisi walipokuja kuchukua hizi maiti hakuna hata mtu mmoja aliyeruhusiwa kusogelea na kupiga picha tulishangaa sana kuona jana ulinzi mkali tofauti na siku zote na aliyebainika amepiga alipokonywa simu yake," amesema Ally. Mfanyabiashara mwingine Issa Isaya amesema cha kushangaza maiti zinazookotwa ni za kiume pekee hivyo wanaishi kwa wasiwasi kwa kuwa kila wiki wanakuta maiti zikiwa zinaelea kwenye maeneo hayo. Amesema Septemba 20 mwaka huu maeneo hayo iliokotwa maiti ya kiume iliyofungwa kwenye kiroba ambayo ilikuwa imeharibika . Isaya amesema maiti hiyo iligunduliwa na wavuvi waliokuwa wanavua samaki ambao huwa wanatoa taarifa kwa wafanyabiashara wa eneo hilo. Amesema mwanzo alikuwa anapata shida alipokuwa anaona maiti katika eneo hilo hivyo kwa kuwa kila wiki wanaokota maiti amelazimika kuizoea hali hiyo. Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Murilo Jumanne amesema tukio hilo atazungumzia Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa. Alipotafutwa Kamanda Mambosasa amesema hajapata taarifa ya kuokotwa maiti hizo hivyo anafanyia uchunguzi na atalitolea ufafanuzi leo. "Sina taarifa na hilo hivyo nalifanyia kazi taarifa nitatoa kesho," alisema Mambosasa

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewataka wakuu wa mikoa na wilaya kuacha tabia ya kuwaweka mahabusu watumishi wa umma kwa makosa ya kitaaluma.
Ummy ametoa wito huo leo Jumatatu mjini Bagamoyo wakati akizindua majengo ya wodi ya wazazi na matibabu ya dharura katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo ambayo yamejengwa kwa udhamini wa Taasisi ya Kiisilam ya Dhi Nureyn.
Tukio hilo lilishuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majidi Mwanga na Mbunge wa Bagamoyo, Dk Shukuru Kawabwa, madiwani na viongozi wa CCM wa wilaya hiyo.
Ummy amesema makosa kama hayo yanapaswa kushughulikiwa na mamlaka wanazofanya kazi lakini kitendo cha kuwaweka ndani kinawaondolea morali na ari ya kufanya kazi.
"Nakushukuru Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo sijawahi kusikia umefanya kitendo cha namna hiyo. Ukiona makosa ya kitaaluma wewe walete juu tutawashughulikia," amesema Ummy.
Amesema katika utumishi wake kama waziri amekusudia kuacha kumbukumbu katika kuimarisha afya ya uzazi na mtoto.
"Ndiyo maana katika ziara zangu huwezi kuniona nimeingia kwenye 'general ward' au wodi ya wanaume badala yake napita katika wodi ya wazazi, watoto na famasi sio kwamba wanaume nawadharau hapana, mambo ni mengi na huwezi kuyashika yote kwa pamoja mimi nimeamua kujikita katika kuimarisha afya ya uzazi na watoto," amesema.
Maiti za wanaume watatu zimekutwa pembezoni mwa Bahari ya Hindi eneo la Coco Beach ambapo kati ya hizo moja imekutwa na jiwe kubwa lililofungwa na kamba. Wafanyabiashara wa mihogo wa eneo hilo wamesema juzi wakiwa kwenye biashara zao asubuhi ghafla waliona maiti moja ikielea karibu na miti aina ya mikoko ikiwa na jiwe lililofungwa kifuani huku mikono yake ikifungwa na kamba. Mmoja wa wafanyabiashara, Aziza Ally amesema baada ya kuona maiti hiyo walitoa taarifa polisi ambapo walifika saa 4 asubuhi na kuichukua kwenye gari lao. Amesema ilipofika saa 8 mchana waliona maiti mbili kila moja ikiwa kwenye kiroba zikielea ndipo mmoja wao alitoa taarifa polisi baadaye zilichukuliwa. "Polisi walipokuja kuchukua hizi maiti hakuna hata mtu mmoja aliyeruhusiwa kusogelea na kupiga picha tulishangaa sana kuona jana ulinzi mkali tofauti na siku zote na aliyebainika amepiga alipokonywa simu yake," amesema Ally. Mfanyabiashara mwingine Issa Isaya amesema cha kushangaza maiti zinazookotwa ni za kiume pekee hivyo wanaishi kwa wasiwasi kwa kuwa kila wiki wanakuta maiti zikiwa zinaelea kwenye maeneo hayo. Amesema Septemba 20 mwaka huu maeneo hayo iliokotwa maiti ya kiume iliyofungwa kwenye kiroba ambayo ilikuwa imeharibika . Isaya amesema maiti hiyo iligunduliwa na wavuvi waliokuwa wanavua samaki ambao huwa wanatoa taarifa kwa wafanyabiashara wa eneo hilo. Amesema mwanzo alikuwa anapata shida alipokuwa anaona maiti katika eneo hilo hivyo kwa kuwa kila wiki wanaokota maiti amelazimika kuizoea hali hiyo. Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Murilo Jumanne amesema tukio hilo atazungumzia Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa. Alipotafutwa Kamanda Mambosasa amesema hajapata taarifa ya kuokotwa maiti hizo hivyo anafanyia uchunguzi na atalitolea ufafanuzi leo. "Sina taarifa na hilo hivyo nalifanyia kazi taarifa nitatoa kesho," alisema Mambosasa Maiti za wanaume watatu zimekutwa pembezoni mwa Bahari ya Hindi eneo la Coco Beach ambapo kati ya hizo moja imekutwa na jiwe kubwa lililofungwa na kamba.  Wafanyabiashara wa mihogo wa eneo hilo wamesema juzi wakiwa kwenye biashara zao asubuhi ghafla waliona maiti moja ikielea karibu na miti aina ya mikoko ikiwa na jiwe lililofungwa kifuani huku mikono yake ikifungwa na kamba.  Mmoja wa wafanyabiashara, Aziza Ally amesema baada ya kuona maiti hiyo walitoa taarifa polisi ambapo walifika saa 4 asubuhi na kuichukua kwenye gari lao.  Amesema ilipofika saa 8 mchana waliona maiti mbili kila moja ikiwa kwenye kiroba zikielea ndipo mmoja wao alitoa taarifa polisi baadaye zilichukuliwa.  "Polisi walipokuja kuchukua hizi maiti hakuna hata mtu mmoja aliyeruhusiwa kusogelea na kupiga picha tulishangaa sana kuona jana ulinzi mkali tofauti na siku zote na aliyebainika amepiga alipokonywa simu yake," amesema Ally.  Mfanyabiashara mwingine Issa Isaya amesema cha kushangaza maiti zinazookotwa ni za kiume pekee hivyo wanaishi kwa wasiwasi kwa kuwa kila wiki wanakuta maiti zikiwa zinaelea kwenye maeneo hayo.  Amesema Septemba 20 mwaka huu maeneo hayo iliokotwa maiti ya kiume iliyofungwa kwenye kiroba ambayo ilikuwa  imeharibika .  Isaya amesema maiti hiyo iligunduliwa na wavuvi waliokuwa wanavua samaki ambao huwa wanatoa  taarifa kwa wafanyabiashara wa eneo hilo.  Amesema mwanzo alikuwa anapata shida alipokuwa anaona maiti katika eneo hilo hivyo kwa kuwa kila wiki wanaokota maiti amelazimika kuizoea hali hiyo.  Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Murilo Jumanne amesema tukio hilo atazungumzia Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa.  Alipotafutwa Kamanda Mambosasa amesema hajapata taarifa ya kuokotwa maiti hizo hivyo anafanyia uchunguzi na atalitolea ufafanuzi leo.     "Sina taarifa na hilo hivyo nalifanyia kazi taarifa nitatoa kesho," alisema Mambosasa Reviewed by EXUPER ASSOCIATION on September 25, 2017 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.