To Advertise here call +255786419829

To Advertise here call +255786419829

Kenya:Mahakama yasikiza kesi inayopinga uchaguzi wa Uhuru Kenyatta


Mahakama ya juu nchini Kenya inasikiliza kesi ya kupinga ushindi wa Uhuru Kenyatta
Image captionMahakama ya juu nchini Kenya inasikiliza kesi ya kupinga ushindi wa Uhuru Kenyatta

Kwa mara ya pili katika chini ya kipindi cha miezi mitatu, macho yote sasa yanaangazia mahakama ya upeo wa juu zaidi Kenya, itakayoamua iwapo ushindi wa rais Kenyatta, ni halali au la.
Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais Kenya na tume ya Uchaguzi IEBC, baada ya uchaguzi wa marudio ya Oktoba 26.
Kesi tatu zimewasilishwa mbele ya majaji 6 wanaoongozwa na jaji mkuu David Maraga, mbili zikitaka ushindi wa rais Kenyatta ubatilishwe, huku moja ikitaka viongozi wa upinzani wakiongozwa na Raila Odinga wachukuliwe hatua kwa madai ya kuchochea wafuasi wao kususia uchaguzi, na kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi.

Rais Uhuru Kenyatta
Image captionRais Uhuru Kenyatta

Kesi za kubatilisha ushindi wa rais Kenyatta zimewasilishwa kwa misingi kwamba tume ya uchaguzi ilikosa kuagiza uteuzi mpya wa chama ufanyike baada ya mahakama ya upeo wa juu zaidi kufutilia mbali ushindi wa rais Kenyatta mwezi Agosti.
Mahakama ina chini ya siku saba kusikiliza na kuamua kesi hizo tatu.

Kiongozi wa upinzani nchini humo alisusia uchaguzi huo
Image captionKiongozi wa upinzani nchini humo alisusia uchaguzi huo

Uamuzi rasmi unatarajiwa kutolewa tarehe 21 mwezi huu.
Kenya:Mahakama yasikiza kesi inayopinga uchaguzi wa Uhuru Kenyatta Kenya:Mahakama yasikiza kesi inayopinga uchaguzi wa Uhuru Kenyatta Reviewed by EXUPER ASSOCIATION on November 15, 2017 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.