To Advertise here call +255786419829

To Advertise here call +255786419829

M/kiti wa Kijiji cha Ililika, Wananchi wamrejesha baada ya kubaini walikosea kumngo’a

Image result for KIJIJI CHA ILILIKA PICHAKATIKA hali isiyokuwa ya kawaida wananchi wa kijiji cha Ililika Kata ya Nyarugusu Wilayani Geita wameamua kumrejesha madarakani Mwenyekiti wao wa Kijiji hicho Daniel Ngíwigulu baada ya kubaini walifanya makosa kumg’oa kwenye nafasi hiyo kwa tuhuma ambazo hazikuwa na chembe ya ukweli miezi mitano iliyopita licha ya kinachodaiwa maendeleo aliyoyafanya katika kipindi kifupi cha uongozi wake.
Kurejeshwa kwa mwenyekiti huyo kumeshuhudiwa na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali mbele ya mkuu wa Wilaya hiyo Herman Kapufi aliyeombwa na wananchi hao kukubali maombi yao ya kumrejesha mwenyekiti wao kwani walichukua maamuzi hayo kwa kukurupuka ( huku wakidai kuwa tangu dunia iumbwe hawajawahi kuona mwenyekiti mchapakazi kama Ngíwigulu hali iliyomfanya mkuu huyo wa wilaya akubali maombi yao huku akiwataka kuchapa kazi na si kuendekeza majungu).
Awali kabla ya tukio hilo,mkuu huyo wa wilaya aliyefanya ziara ya kikazi kwenye kata hiyo alitembelea shule ya Msingi Torogo iliyojengwa na Mwekezaji mzawa Evarist Gervas kwa kushirikiana na wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu.
M/kiti wa Kijiji cha Ililika, Wananchi wamrejesha baada ya kubaini walikosea kumngo’a M/kiti wa Kijiji cha Ililika, Wananchi wamrejesha baada ya kubaini walikosea kumngo’a Reviewed by EXUPER ASSOCIATION on November 14, 2017 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.