Wakazi wa jiji la Dsm wametakiwa kujitokeza kuanzia Nov.20 katika Upimaji Afya kwenye meli kubwa ya Jeshi la majini la China
Mkuu wa Mkoa wa Dsm Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari pamoja na makamanda wa jeshi la Majini la China ambao tayari wamewasili amesema,kuwasili kwa meli hiyo kutokana na balozi wa China aliyemaliza Muda wake Dr.LU ambae alijionea mafuriko ya wananchi katika Upimaji afya katika Viwanja vya Mnazi mmoja miezi mitatu iliyopita na Kuahidi kuleta madaktari kuunga Mkono jitihada za Bw,Makonda.
Aidha makonda amewataka wananchi waliokuwa wakisubiri kufanyiwa Upasuaji katika hospitali za m/myamala,temeke na amana ambao wako katika foleni ya kusubiri kufika katika meli hiyo ili kufanyiwa upasuaji huku ikiwa na Vifaa vya kisasa vya Tiba.
Meja Chi Song Kutoka katika kikosi cha jeshi la majini katika meli hiyo ambayo ni kubwa kuliko meli zote zilizowahi kuingia hapa nchini amesema Matibabu hayo ya bure ni matokeo mazuri ya Ushirikiano katika ya Tanzania na China pamoja na waasisi wa nchini hizo.
Wakazi wa jiji la Dsm wametakiwa kujitokeza kuanzia Nov.20 katika Upimaji Afya kwenye meli kubwa ya Jeshi la majini la China
Reviewed by EXUPER ASSOCIATION
on
November 14, 2017
Rating:
No comments: