To Advertise here call +255786419829

To Advertise here call +255786419829

Wananchi Mbarali Walalamikia Agizo la DC Kuchukua Eneo la Kilimo

Image result for Wananchi Mbarali WalalamikiaWANANCHI wanaoishi eneo la Katenge, Kitongoji ya Tembo B Mtaa wa Nyeregete katika Mamlaka ya Mji mdogo wa Rujewa Wilayani Mbarali, wamelalamikia agizo la Mkuu wa Wilaya ya Mbarali la kupima eneo la katenge na kugawa ardhi kwa vijana kwa ajili ya kilimo, wakidai kuwa hawakushirikishwa kufikia maamuzi.
Aidha wananchi hao wanahofu ya kuondolewa kwenye maeneo yao endapo agizo hilo litatekelezwa, wakidai kuwa katika orodha ya watakaogawiwa ardhi ya kilimo baada ya upimaji wao hawamo.
Channel Ten ikazungumza na Afisa Mtendaji wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Rujewa Fortunatus Mjengwa,naye akasema mgogoro huo ni wa muda murefu , na kwamba yeye anatekeleza agizo la Mkuu wa Wilaya lakini pia akasema taratibu zote za kisheria zimefuatwa.
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Rubein Mfune anasema Uamuzi huo umefikiwa baada ya kuwa na ushirikishwaji wa pamoja.
Wananchi Mbarali Walalamikia Agizo la DC Kuchukua Eneo la Kilimo Wananchi Mbarali Walalamikia Agizo la DC Kuchukua Eneo la Kilimo Reviewed by EXUPER ASSOCIATION on November 14, 2017 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.