To Advertise here call +255786419829

To Advertise here call +255786419829

Rais Mwinyi amtembelea Lissu hospitalini

Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi amemtembelea mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyelazwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya.
Rais Mwinyi akiambatana na mke wake na maofisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Kenya, wamemtembelea Lissu hospitalini hapo alipolazwa tangu Septemba 7  anakotibiwa baada ya kuuguza majeraha ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma.
Rais Mwinyi anakuwa miongoni mwa viongozi wa juu wa Serikali waliomtembelea Lissu ambaye ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) ambaye hivi karibuni Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan naye alifika hospitalini hapo kumjulia hali.
Mwisho
Rais Mwinyi amtembelea Lissu hospitalini Rais Mwinyi amtembelea Lissu hospitalini Reviewed by EXUPER ASSOCIATION on December 05, 2017 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.