
Mbunge wa Kibamba, John Mnyika amesema taarifa kwamba amejiuzulu nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Chadema -Bara hazina ukweli.
Mnyika ambaye amekuwa akitajwa tajwa kwamba atakihama chama hicho, ametoka kauli hiyo baada ya kuwapo taarifa kwamba amejiuzulu wadhifa huo.
Akizungumza leo Jumanne Desemba 5,2017 jioni kuhusu taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba amejiuzulu; Mnyika amesema, ‘’Si kweli ni taarifa za uongo.’’
Mnyika: Sijajiuzulu wadhifa wangu Chadema
Reviewed by EXUPER ASSOCIATION
on
December 05, 2017
Rating:
No comments: