To Advertise here call +255786419829

To Advertise here call +255786419829

Uhuru waahirisha mkutano wa Chadema na waandishi wa habari


 Katika hali isiyo ya kawaida, lakini ya kuunga mkono mshikamano, jana Chadema iliahirisha mkutano wake na waandishi wa habari kupisha tukio la kitaifa la kuadhimisha miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Sherehe za Uhuru huadhimishwa Desemba 9 ya kila mwaka na huhudhuriwa na wananchi, viongozi wa Serikali, vyama vya siasa na mabalozi waliopo nchini.
Kwa miaka kadhaa sasa baadhi ya viongozi wa upinzani hasa wa vyama vikubwa wamekuwa ‘wakisusia’ shehere hizo kutokana na misuguano ya kisiasa.
Juzi, Chadema ilitoa mwaliko kwa vyombo vya habari kwamba jana wangetoa taarifa kuhusiana na maazimio ya kikao cha Kamati Kuu, lakini hali haikuwa hivyo.
Katika hali isiyo ya kawaida mkutano huo ulifutwa na badala yake imetangazwa utafanyika leo.
Mkutano huo ulilenga kuzungumza mambo kadhaa ikiwamo uchaguzi wa marudio wa majimbo matatu ya Songea Mjini (Ruvuma), Singida Kaskazini (Singida) na Longido mkoani Arusha.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imeyatangaza majimbo hayo matatu kuwa yapo wazi.
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema visiwani Zanzibar, Salum Mwalimu aliliambia gazeti hili jana kuwa wameshindwa kufanya mkutano huo kwa sababu mbalimbali ikiwamo maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
“Kuna vitu havijakaa sawa, tunaendelea kuvikamilisha na kesho (leo), tutazungumza na waandishi wa habari tukiwa tumekamilisha kila kitu,” alisema Mwalimu huku akimtaka mwandishi kuwa mvumilivu kwani kila kitu kitajulikana leo kwa kuwa Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe ndiye atakayezungumza.

Uhuru waahirisha mkutano wa Chadema na waandishi wa habari Uhuru waahirisha mkutano wa Chadema na waandishi wa habari Reviewed by EXUPER ASSOCIATION on December 09, 2017 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.