
Mkuu wa Mkoa wa Manyara mstaafu, Joel Bendera aliyefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Jumatano Desemba 6,2017 anazikwa leo wilayani Korogwe.
Kwa mujibu wa ratiba, mazishi yatafanyika mchana wa leo Jumapili Desemba 10,2017.
Viongozi mbalimbali wamefika nyumbani kwa marehemu kuaga mwili. Miongoni mwao ni Rais mstaafu Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi.
Wengine ni Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo; Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira; Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba; na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), Wales Karia.
Bendera pia amewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. Mbali ya ukuu wa mkoa, amewahi kuwa mbunge wa Korogwe Mjini na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo katika utawala uliopita wa Rais mstaafu, Kikwete.
Katika mabadiliko ya wakuu wa mikoa yaliyofanywa na Rais John Magufuli Oktoba 26,2017, Bendera alikuwa miongoni mwa waliostaafu.
Nafasi yake imechukuliwa na Alexander Mnyeti aliyepandishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara akitokea kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.
Wengi wajitokeza mazishi ya Bendera Korogwe
Reviewed by EXUPER ASSOCIATION
on
December 10, 2017
Rating:
No comments: