To Advertise here call +255786419829

To Advertise here call +255786419829

VIDEO-Mwongozo huduma za maji wazinduliwa

 Serikali imezindua mwongozo wa huduma za maji na usafi wa mazingira katika vituo vya tiba.
Mwongozo huo kwa zahanati, vituo vya afya na hospitali ni katika kuelekea uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira.
Mkurugenzi wa idara ya uratibu wa sekta kutoka Tamisemi, Dk Andrew Komba amesema uzinduzi wa mwongozo huo ni kueleka awamu ya pili ya kampeni itakayozinduliwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan Desemba 7,2017 mjini Dodoma.
Mratibu wa kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira, Anyitike Mwakitalima amesema kutokana na kulegalega katika baadhi ya maeneo, waligundua kisababishi kimojawapo ni ukosefu wa mwongozo wa Taifa ambao wadau na Serikali wangeutumia kusimamia usafi wa mazingira.
Amesema malengo ya kitaifa ni ifikapo Juni 2021 kuhakikisha hakuna kaya isiyo na choo.
Mkurugenzi wa mipango kutoka Shirika la Water Aid, Abel Duganga amesema kukosekana kwa mwongozo unaopima hali ya maji nchini, utendaji wa Serikali na wadau ulikuwa ukisuasua, lakini sasa utawezesha kuwa na vigezo vinavyofanana katika kupima na kuwa na takwimu sahihi.
VIDEO-Mwongozo huduma za maji wazinduliwa VIDEO-Mwongozo huduma za maji wazinduliwa Reviewed by EXUPER ASSOCIATION on December 05, 2017 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.