
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William ole Nasha amesema Serikali imejipanga kwa ajira za wahitimu wa vyuo vya ufundi.
Akizungumza katika chuo cha Veta Moshi amesema kutokana na mafundi kuhitajika sehemu mbalimbali watahakikisha wahitimu wanapata ajira.
"Elimu ya ufundi ni ya muhimu ndiyo maana kwa kulitambua hilo, Serikali imeelekeza nguvu huko. Msihofu someni na kama hamtaajiriwa basi jiajirini," amesema.
Amesema mafundi wanahitajika kwa ajili ya ujenzi wa reli na miradi mingine.
Ole Nasha amewataka vijana kuondokana na dhana kwamba elimu ya ufundi ni kwa mtoto wa kiume pekee, kwa kuwa hata watoto wa kike wana fursa ya kupata elimu hiyo.
Amesema suala la kusoma hadi chuo kikuu si mwisho wa kujifunza, hivyo amewataka wanafunzi kusomea masuala ya ufundi ili waweze kujiajiri na kuajiriwa.
Akisoma taarifa, kaimu mkuu wa Chuo cha Veta Moshi, Douglas Mlula amesema kinakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia na miundombinu.
Ameiomba Serikali kuondoa kodi wanaponunua vifaa kwa kuwa wanayotozwa ni kubwa na inawafanya washindwe kuvinunua.
Wahitimu Veta wahakikishiwa ajira
Reviewed by EXUPER ASSOCIATION
on
December 04, 2017
Rating:
No comments: