To Advertise here call +255786419829

To Advertise here call +255786419829

Kampeni ya ujenzi wa ofisi za walimu DSM, kupitia vibox vya CRDB umezinduliwa rasmi leo na Paul Makonda

Image result for MAKONDA NA CRDBKampeni ya ujenzi wa ofisi za walimu mkoa wa Dar e salaam kupitia vibox vilivyowekwa kwenye matawi yote ya benki ya CRDB umezinduliwa rasmi leo na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, ambapo katika kipindi cha wiki tatu toka vibox hivyo viwekwe kwenye matawi jumla ya shilingi millioni kumi na tano zimepatikana.
Akiongea kwenye uzinduzi huo makao makuu ya benki ya Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Dk Kimei amesema, benki yake imeamua kuingia kwa asilimia mia moja kwenye kampeni hiyo kwa sababu ya kutambua umuhimu wa walimu katika kujenga misingi ya taifa katika nyanja zote ikiwemo watalaam, uchumi pamoja na mustakabali wa nchi kwa ujumla.
Mkuu wa mkoa wa dar es salaam, Paul Makonda ameshindwa kuficha hisia za furaha aliyokuwa nayo kutokana na jitihada hizo za benki ya CRDB za kuhakikisha zoezi la ujenzi wa ofisi za walimu mkoani dar es salaam linafanikiwa.
Mkuu wa mkoa huyo amewataka watanzania kutambua kuwa pamoja na kuwa ualimu ni wito, lakini wito kwenye mazingira magumu hufanya kazi kuwa ngumu zaidi, hivyo ameendelea kuwaomba watanzania kila moja kwa nafasi yake na uwezo wake kuchangia kwa faida ya watanzania wenyewe na taifa kwa ujumla.
Katika kuendelea kuhamasisha watanzania kuchangia kampeni hiyo ambayo moja wa wadau wake wakuu ni kituo cha Television cha Channel Ten kituo ambacho kimejitolea kutangaza matangazo ya kampeni hiyo bure, mkuu wa mkoa alichangia kwenye vibox hivyo shilingi laki nne na hivyo kuhamasisha wateja mbalimbali waliokuwepo kwenye moja ya tawi la benki ya CRDB nao kuchangia.

Kampeni ya ujenzi wa ofisi za walimu DSM, kupitia vibox vya CRDB umezinduliwa rasmi leo na Paul Makonda Kampeni ya ujenzi wa ofisi za walimu DSM, kupitia vibox vya CRDB umezinduliwa rasmi leo na Paul Makonda Reviewed by EXUPER ASSOCIATION on November 14, 2017 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.